Report, if you have a problem with this page“ Kuna nguzo saba ambazo hazina budi kuzingatiwa kama unataka kuheshimiwa na kuwaheshimu wengine. Kwanza kabisa jitambue: wewe ni nani na unafanya nini hapa duniani. Halafu, kabla ya kusema jambo lolote kwa mtu yoyote fikiria kwanza maana au madhara ya hilo unalotaka kulisema. Kisha jifunze tamaduni mbalimbali na watendee wengine kama vile unavyotaka kutendewa au kama vile wanavyotaka kutendewa. Jifunze kusamehe na kusuluhisha migogoro katika jamii unamoishi huku ukidumisha heshima na utu kwa binadamu wenzako. Jijengee imani kwa watu, punguza upendeleo, fanya kazi kama timu kwani hakuna ‘mimi’ katika umoja ila kuna ‘sisi’, na jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE kwa manufaa ya wote. Kuwa kiongozi katika kila jambo unalofanya na katika kila kitu unachofanya. Jitahidi kufanya jambo au kitu kwa usahihi kwa kadiri utakavyoweza. ”